Isaiah 41:8-10


8 a“Lakini wewe, ee Israeli, mtumishi wangu,
Yakobo, niliyemchagua,
ninyi wazao wa Ibrahimu rafiki yangu,

9 bnilikuchukua toka miisho ya dunia,
nilikuita kutoka pembe zake za mbali.
Nilisema, ‘Wewe ni mtumishi wangu’;
nimekuchagua, wala sikukukataa.

10 cHivyo usiogope, kwa maana niko pamoja nawe;
usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako.
Nitakutia nguvu na kukusaidia;
nitakutegemeza kwa mkono wa kuume wa haki yangu.

Copyright information for SwhKC